Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 22 · Aya ya 71

Al-Hajj 22:71

الحج

وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِۦ سُلْطَـٰنًا وَمَا لَيْسَ لَهُم بِهِۦ عِلْمٌ ۗ وَمَا لِلظَّـٰلِمِينَ مِن نَّصِيرٍ

Maana

Na wanaabudu badala ya Mwenyezi Mungu ambavyo hakuviteremshia ushahidi, na ambavyo hawana elimu navyo. Na madhalimu hawatakuwa na wa kuwasaidia.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wanaabudu badala ya Mwenyezi Mungu ambavyo hakuviteremshia ushahidi, na ambavyo hawana ujuzi navyo. Na madhaalimu hawatakuwa na wa kuwasaidia. [71]

[71] Na washirikina huabudu badala ya Mwenyezi Mungu masanamu na watu ambao haikuteremka hoja yoyote ya kuwaabudu hao katika Kitabu cha mbinguni chochote. Wala wao hawana ushahidi wowote wa kuingia akilini. Lakini wanafanya yote hayo kufuata pumbao na mila tu. Wala hao washirikina walio zidhulumu nafsi zao na wakazidharaulisha akili zao hawato pata msaidizi wa kuwanusuru, na kuwakinga na adhabu ya Moto Siku ya Kiyama, kama wanavyo jidai.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na makafiri wa Kikureshi wanashikilia kumshirikisha Allah Mtukufu pamoja na kuwa ubatilifu wa waliyonayo uko waziwazi. Wao wanawaabudu waungu ambao haukuteremka, kwenye kitabu chochote miongoni mwa vitabu vya Allah Mtukufu, ushahidi kuwa wao wanafaa kufanyiwa ibada, na wao (hao waungu) hawajui chochote kuhusu yale waliyoyazua (hao makafiri) na kumsingizia Allah Mtukufu, hakika hilo ni jambo ambalo kwalo wamewafuata baba zao bila dalili yoyote. Basi kitakapokuja kipindi cha kuhesabiwa huko Akhera, hawa washirikina hawatakuwa na msaidizi mwenye kuwanusuru au kuwakinga na adhabu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hajj

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net