Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 22 · Aya ya 74

Al-Hajj 22:74

الحج

مَا قَدَرُوا۟ ٱللَّهَ حَقَّ قَدْرِهِۦٓ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَقَوِىٌّ عَزِيزٌ

Maana

Hawakumpa taadhima Mwenyezi Mungu anavyostahiki kupewa taadhima. Hakika Mwenyezi Mungu bila ya shaka ni Mwenye nguvu, Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hawakumuadhimisha Mwenyezi Mungu anavyo stahiki kuadhimishwa. Hakika Mwenyezi Mungu bila ya shaka ni Mwenye kushinda. [74]

[74] Hawa washirikina hawamjui Mwenyezi Mungu kama anavyo faa kujuulikana, wala hawamtukuzi kama anavyo stahiki kutukuzwa, walipo kwenda kumshirikisha katika ibada na vitu visio kuwa na maana kabisa. Na hali kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Muweza wa kila kitu, Asiye shindika na yeyote.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hawa washirikina hawakumtukuza Allah Mtukufu vile Anavyostahiki kutukuzwa, kwa kuwa wao wamemfanya kuwa Ana washirika, na hali Yeye Ndiye Mwenye nguvu Aliyeumba kila kitu, Ndiye Mshindi Asiyeshindwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hajj

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net