Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 22 · Aya ya 68

Al-Hajj 22:68

الحج

وَإِن جَـٰدَلُوكَ فَقُلِ ٱللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا تَعْمَلُونَ

Maana

Na wakikujadili, basi sema: Mwenyezi Mungu anajua zaidi mnayoyatenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wakikujadili basi sema: Mwenyezi Mungu anajua zaidi mnayo yatenda. [68]

[68] Na wakishikilia kuendea kukujadili basi waachilie mbali, na waambie: Mwenyezi Mungu anajua zaidi vitendo vyenu, na malipo mnayo yastahiki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wakishikilia kujadiliana na wewe kwa njia ya ubatilifu kuhusu yale unayowalingania nayo, usijadiliane na wao, bali waambie, «Allah Mtukufu ni mjuzi zaidi wa mnayoyafanya ya ukafiri na kukanusha,» kwani wao wanafanya inadi na kiburi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hajj

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net