Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 22 · Aya ya 67

Al-Hajj 22:67

الحج

لِّكُلِّ أُمَّةٍ جَعَلْنَا مَنسَكًا هُمْ نَاسِكُوهُ ۖ فَلَا يُنَـٰزِعُنَّكَ فِى ٱلْأَمْرِ ۚ وَٱدْعُ إِلَىٰ رَبِّكَ ۖ إِنَّكَ لَعَلَىٰ هُدًى مُّسْتَقِيمٍ

Maana

Kila umma tumewawekea ibada zao wanazozishika. Basi wasizozane nawe katika jambo hili. Na waite watu kwenda kwa Mola wako Mlezi. Hakika wewe uko kwenye uongofu ulionyooka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kila umma tumewajaalia na ibada zao wanazo zishika. Basi wasizozane nawe katika jambo hili. Na waite watu kwendea kwa Mola wako Mlezi. Hakika wewe uko kwenye Uwongofu Ulio Nyooka. [67]

[67] Tumewajaalia katika kila umma walio kwisha tangulia wawe na sharia zao makhsusi zinazo ambatana na zama zao, za kumuabudia Mwenyezi Mungu, mpaka zinapo kuja futwa na zijazo baadae. Na kwa hivyo tumewajaalia watu wako, ewe Nabii, wawe na Sharia ya kumuabudu Mwenyezi Mungu mpaka Siku ya Kiyama. Ilivyo kuwa hivi ndio amri yetu na mpango wetu, basi hao wanao jiabudia kwa dini zao zilizo pita, haiwafalii wao kutia mkazo katika kukupinga wewe. Kwani hakika sharia yako wewe imefuta sharia zao. Basi usijishughulishe na kujadiliana nao. Nawe endelea kuwaita watu wende kwa Mola wako Mlezi kwa mujibu wa unavyo pewa wahyi (ufunuo). Hakika wewe unafuata Uwongofu Ulio Nyooka wa Mola wako Mlezi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kila watu miongoni mwa jinsi za watu waliopita tumewawekea sheria na ibada tuliowaamrisha wao kwazo, na wao ni wenye kuzitumia, basi wasikufanyie ushindani, ewe Mtume, hao washirikina wa Kikureshi kuhusu Sheria yako na yale Aliyokuamrisha Allah Mtukufu katika matendo ya Hija na aina zote za ibada. Na ulinganie kwenye kumpwekesha Mola wako na kumtakasia ibada na kufuata amri Yake. Hakika wewe uko kwenye Dini iliyolingana sawa, isiyokuwa na kona kona.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hajj

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net