Al-Hajj 22:69
الحجٱللَّهُ يَحْكُمُ بَيْنَكُمْ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ فِيمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ
Mwenyezi Mungu atahukumu baina yenu Siku ya Kiyama katika hayo mnayohitilafiana.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mwenyezi Mungu atahukumu baina yenu Siku ya Kiyama katika hayo mnayo khitalifiana. [69]
[69] Mwenyezi Mungu atahukumu baina yangu na nyinyi Siku ya Kiyama katika hayo mnayo khitalifiana nami. Atamlipa thawabu aliye ongoka na atamuadhibu aliye potoka.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Atahukumu kati ya Waislamu na makafiri Siku Ya Kiyama katika tafauti zao kuhusu dini. Katika aya hii pana adabu nzuri ya kuwarudi wanaofanya mjadala kwa njia ya ujeuri na kiburi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net