Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 22 · Aya ya 62

Al-Hajj 22:62

الحج

ذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلْحَقُّ وَأَنَّ مَا يَدْعُونَ مِن دُونِهِۦ هُوَ ٱلْبَـٰطِلُ وَأَنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلْعَلِىُّ ٱلْكَبِيرُ

Maana

Hayo ni kwa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye wa kweli, na kwamba wale wanaowaomba badala yake, ni batili, na hakika Mwenyezi Mungu ndiye aliye juu, Mkubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hayo ni kwa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Wa Kweli, na kwamba wale wanao waomba badala yake, ni baat'ili, na hakika Mwenyezi Mungu ndiye Aliye Juu na ndiye Mkubwa. [62]

[62] Huo ndio msaada wa wenye kudhulumiwa unao tokana na Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na kutenda kwake katika ulimwengu kama atakavyo bila ya kiwango ni kama muonavyo matokeo yake; na kwa hakika Yeye ndiye Mungu wa Haki ambaye hapana mungu mwenginewe pamoja naye. Na kwamba masanamu wanayo yaabudu washirikina ni uwongo, hayana ukweli, na Mwenyezi Mungu peke yake ndiye aliye tukuka juu ya vyote isipo kuwa Yeye Mwenyewe kwa shani yake, na ni Mkuu wa madaraka.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hayo ni kwamba Allah Mtukufu Ndiye Mola wa haki Ambaye hapana yoyote Anayepasa aabudiwe isipokuwa Yeye, na kwamba vile wanavyoviabudu washirikina miongoni mwa masanamu na waungu bandia wanaodaiwa kufanana na Yeye ndio batili wasionufaisha wala kudhuru, na kwamba Allah Mtukufu Ndiye Aliye juu ya viumbe vyake kwa dhati, cheo na utendeshaji nguvu, Ndiye aliyetakasika na wanaodaiwa kufanana na Yeye na kuwa wendani Wake, Aliye Mkuu katika dhati Yake, majina Yake na sifa Zake. Yeye ni Mkubwa kuliko kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hajj

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net