Al-Hajj 22:61
الحجذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱللَّهَ يُولِجُ ٱلَّيْلَ فِى ٱلنَّهَارِ وَيُولِجُ ٱلنَّهَارَ فِى ٱلَّيْلِ وَأَنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌۢ بَصِيرٌ
Hayo ni kwa kuwa Mwenyezi Mungu huingiza usiku katika mchana, na huuingiza mchana katika usiku, na ya kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hayo ni kwa kuwa Mwenyezi Mungu huingiza usiku katika mchana, na huuingiza mchana katika usiku, na ya kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kuona. [61]
[61] Msaada huo ni mwepesi kwa Mwenyezi Mungu, kwani Yeye ni Muweza wa kila kitu. Na katika Ishara za uwezo wake zilio wazi mbele yenu ni utawala wake juu ya ulimwengu wote. Huzungusha usiku na mchana, pengine huzidi huu au huzidi huu. Inakuwa baadhi ya kiza cha usiku pahala pa mwanga wa mchana. Na pengine huwa kinyume cha hivyo. Naye Subhanahu juu ya uwezo wake husikiliza kauli ya aliye dhulumiwa, na anaviona vitendo vya mwenye kudhulumu. Basi humtia adhabuni.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Huyo aliyewawekea hukumu hizo za uadilifu Ndiye wa kweli, na Yeye Ndiye Muweza wa alitakalo. Na katika uwezo Wake ni kwamba Yeye Anaziingiza saa za usiku zipunguazo kwenye saa za mchana, na anaziingiza saa za mchana zipunguazo kwenye saa za usiku, na kwamba Allah Mtukufu ni Msikizi wa kila sauti, ni Muoni wa kila kitendo, hakifichiki kitu chochote Kwake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net