Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 22 · Aya ya 60

Al-Hajj 22:60

الحج

ذَٰلِكَ وَمَنْ عَاقَبَ بِمِثْلِ مَا عُوقِبَ بِهِۦ ثُمَّ بُغِىَ عَلَيْهِ لَيَنصُرَنَّهُ ٱللَّهُ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَعَفُوٌّ غَفُورٌ

Maana

Ndiyo namna hivi. Na anayelipiza mfano wa alivyoadhibiwa, kisha akadhulumiwa, basi hakuna shaka Mwenyezi Mungu atamsaidia. Hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu, Mwenye maghfira.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ndio namna hivi. Na anaye lipiza mfano wa alivyo adhibiwa, kisha akadhulumiwa, basi hapana shaka Mwenyezi Mungu atamsaidia. Hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu Mwenye maghfira. [60]

[60] Huo ndio mwendo wetu katika kuwalipa watu. Hatuwadhulumu. Na Muumini mwenye kulipiza kisasi kwa aliye mfanyia uovu, na akalipiza kwa kadri ya alivyo tendewa bila ya kuzidisha, kisha yule mkosa akaja kumfanyia uadui tena baada yake, basi hakika Mwenyezi Mungu anatoa ahadi ya nguvu kuwa atamnusuru na kumsaidia yule aliye dhulumiwa. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kumsamehe mwenye kulipiza kama alivyo dhulumiwa. Hamtii makosani kwa hayo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, basi huyasitiri makosa ya kuteleza ya mja wake mt'iifu, wala hamfedhehi Siku ya Kiyama.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hilo ni jambo tulilokusimulia la kuwatia Peponi waliohama (katika njia ya Allah Mtukufu), na mwenye kufanyiwa uadui na kuonewa basi yeye ameruhusiwa kupambana na huyo mhalifu kwa kitendo kama chake, na atakuwa hana makosa. Na akirudi yule mhalifu kumuonea na akafanya udhalimu, basi Allah Mtukufu Atampa ushindi yule mdhulumiwa aliyeonewa, kwani haifai afanyiwe uadui kwa kuwa amejilipizia. Hakika Allah Mtukufu ni Msamehefu, ni Mwingi wa kusamehe, Anasamehe dhambi za wenye kukosea, hawafanyii haraka kuwatesa, na anazisitiri dhambi zao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hajj

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net