Al-Hajj 22:59
الحجلَيُدْخِلَنَّهُم مُّدْخَلًا يَرْضَوْنَهُۥ ۗ وَإِنَّ ٱللَّهَ لَعَلِيمٌ حَلِيمٌ
Bila ya shaka atawaingiza mahali watakapoparidhia. Na hakika Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi, Mstahamilivu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
BIla ya shaka atawaingiza pahala watakapo paridhia. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mpole. [59]
[59] Na hakika atawatia katika Pepo kwenye vyeo watavyo ridhika navyo na vitawafurahisha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuzijua vyema hali zao, basi atawalipa malipo bora, naye ni Mpole huyasamehe makosa yao madogo madogo ya kuteleza.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Atawatia Mola wao tena Atawatia mahali pa kuingia ambapo watapapenda, napo ni Peponi. Na kwa hakika Allah Mtukufu Anamjua sana yule anayetoka katika njia Yake, na mwenye kutoka kwa ajili ya ulimwengu, ni Mpole kwa wale waliomuasi hawafanyii haraka kuwatesa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net