Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 22 · Aya ya 58

Al-Hajj 22:58

الحج

وَٱلَّذِينَ هَاجَرُوا۟ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ ثُمَّ قُتِلُوٓا۟ أَوْ مَاتُوا۟ لَيَرْزُقَنَّهُمُ ٱللَّهُ رِزْقًا حَسَنًا ۚ وَإِنَّ ٱللَّهَ لَهُوَ خَيْرُ ٱلرَّٰزِقِينَ

Maana

Na waliohama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kisha wakauawa au wakafa, bila ya shaka Mwenyezi Mungu atawaruzuku riziki njema. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mbora wa wanaoruzuku.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na walio hama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kisha wakauwawa au wakafa, bila ya shaka Mwenyezi Mungu atawaruzuku riziki njema. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mbora wa wanao ruzuku. [58]

[58] Na wenye kuacha nchi zao kwa ajili ya kutukuza shani ya Dini yao wakitafuta radhi za Mwenyezi Mungu, kisha wakauliwa katika uwanja wa Jihadi, au wakafa vitandani mwao, Mwenyezi Mungu atawalipa malipo mazuri kabisa. Na hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mbora wa kutoa thawabu za ukarimu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wale waliotoka majumbani mwao kwa kutaka radhi za Allah Mtukufu na kuinusuru Dini Yake, yoyote kati yao atakayeuawa akiwa katika hali ya kupigana na makafiri, na yoyote kati yao atakayekufa bila kupigana, Allah Mtukufu Atawaruzuku Pepo na starehe zake zisizokatika wala kuondoka. Na kwa hakika, Allah Mtukufu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Ndiye Mbora wa wenye kuruzuku.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hajj

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net