Al-Hajj 22:57
الحجوَٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَكَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا فَأُو۟لَـٰٓئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ
Na waliokufuru na kuzikanusha Ishara zetu, basi hao watapata adhabu ya kufedhehesha.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na walio kufuru na kuzikanusha Ishara zetu, basi hao watapata adhabu ya kufedhehesha. [57]
[57] Na walio kufuru na wakazikanusha Aya za Qur'ani tulizo mteremshia Muhammad, hao watakuta adhabu ya madhila na fedheha.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wale walioukataa upweke wa Allah Mtukufu, wakawakanusha Mitume Wake na wakazipinga aya za Qur’ani, basi hao watapata adhabu yenye kuwafanya wanyonge na kuwatweza ndani ya moto wa Jahanamu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net