Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 22 · Aya ya 63

Al-Hajj 22:63

الحج

أَلَمْ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً فَتُصْبِحُ ٱلْأَرْضُ مُخْضَرَّةً ۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَطِيفٌ خَبِيرٌ

Maana

Je, huoni kwamba Mwenyezi Mungu huteremsha maji kutoka mbinguni, na mara ardhi inakuwa kijani kibichi? Hakika Mwenyezi Mungu ni Mpole, Mwenye habari zote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu huteremsha maji kutoka mbinguni, na mara ardhi inakuwa chanikiwiti? Hakika Mwenyezi Mungu ni Mpole na Mwenye kujua. [63]

[63] Ewe mwenye akili! Huzingatii haya yalio kuzunguka uyaonayo kwa macho yenye kuonyesha uwezo wa Mwenyezi Mungu, ukamuabudu Yeye peke yake? Yeye ndiye anaye iteremsha mvua kutoka mawinguni, na ardhi ikageuka rangi ya kijani kibichi kwa mimea inayo chipuka, baada ya kuwa na ukame. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mpole mno kwa waja wake, na anajua vyema yanayo wanufaisha na kwa hivyo akawatengenezea kwa kudra yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je, huoni, ewe Mtume, kwamba Allah Mtukufu Ameteremsha mvua kutoka mbinguni, ardhi ikawa kijani kwa mimea iliyomea? Hakika Allah Mtukufu ni Mwenye huruma na upole kwa waja Wake, kwa kuitoa mimea kutoka ardhini kwa maji hayo, ni mtambuzi wa mambo yanayowafaa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hajj

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net