Al-Hajj 22:50
الحجفَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ
Basi walioamini na wakatenda mema watapata kufutiwa dhambi na riziki za ukarimu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi walio amini na wakatenda mema watapata maghfira na riziki za ukarimu. [50]
[50] Na wale walio muamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakatenda vitendo vyema, watapata kutokana na Mwenyezi Mungu kusamehewa dhambi zao walizo ziingia, kama kadhaalika watavyo pata riziki ya ukarimu huko Peponi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi wale wenye kumuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake, na imani hiyo ikajikita kwenye nyoyo zao na wakafanya matendo mema, watapata msamaha wa dhambi zao kutoka kwa Mola wao, na sitara ya kufunika matendo ya uasi yaliyotokana na wao na riziki nzuri isiyokatika, nayo ni Pepo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net