Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 22 · Aya ya 49

Al-Hajj 22:49

الحج

قُلْ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِنَّمَآ أَنَا۠ لَكُمْ نَذِيرٌ مُّبِينٌ

Maana

Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni mwonyaji kwenu niliye dhahiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni mwonyaji kwenu niliye dhaahiri. [49]

[49] Ewe Nabii! Waambie hao wanao kanusha, wanao kuhimiza waletewe adhabu: Sio kazi yangu mimi kukulipeni kwa vitendo vyenu. Bali hakika mimi ni mwenye kukuhadharisheni kwa hadhari iliyo wazi kwamba kuna adhabu. Na Mwenyezi Mungu ndiye wa kukuhisabuni na kukulipeni.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, «Enyi watu! Mimi si kuwa isipokuwa ni muonyaji kwenu mwenye kufikisha ujumbe wa Allah Mtukufu».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hajj

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net