Al-Hajj 22:51
الحجوَٱلَّذِينَ سَعَوْا۟ فِىٓ ءَايَـٰتِنَا مُعَـٰجِزِينَ أُو۟لَـٰٓئِكَ أَصْحَـٰبُ ٱلْجَحِيمِ
Na wanaojitahidi kuzipinga Aya zetu, hao ndio watu wa Motoni.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wanao jitahidi kuzipinga Aya zetu hao ndio watu wa Motoni. [51]
[51] Na wale walio jikukusa nafsi zao katika kuipiga vita Qur'ani kushindana na Waumini na kuwapinga, wakitamani na kudai kwa uwongo, kwamba wao watapata wayatakayo - watu hao watabaki milele katika adhabu ya Motoni.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wale wenye kujitahidi kufanya vitimbi ili kuzitengua aya za Qur’ani kwa kuzikanusha hali ya kuwa ni wabishi na washindani, basi hao ndio watu wa Moto wenye kuwaka, wataungia na watasalia humo milele.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net