Al-Hajj 22:23
الحجإِنَّ ٱللَّهَ يُدْخِلُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ جَنَّـٰتٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ يُحَلَّوْنَ فِيهَا مِنْ أَسَاوِرَ مِن ذَهَبٍ وَلُؤْلُؤًا ۖ وَلِبَاسُهُمْ فِيهَا حَرِيرٌ
Hakika Mwenyezi Mungu atawaingiza walioamini na wakatenda mema katika Bustani ambazo mito inapita kati yake. Watapambwa humo kwa mapambo ya mikononi ya dhahabu na lulu. Na mavazi yao humo ni hariri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika Mwenyezi Mungu atawaingiza walio amini na wakatenda mema katika Bustani zipitiwazo na mito kati yake. Watapambwa humo kwa mapambo ya mikononi ya dhahabu na lulu. Na mavazi yao humo ni hariri [23]
[23] Ama walio amini na wakatenda vitendo vyema, hao bila ya shaka Mwenyezi Mungu atawaingiza kwenye Mabustani yanayo pita mito kati ya majumba yake na miti yake. Humo watastarehe kwa kila namna ya starehe, na Malaika watawapamba vikuku vya mikono vya dhahabu na watawapamba kwa lulu. Ama nguo zao za kawaida zitakuwa za hariri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika Allah Mtukufu Atawatia watu wa Imani na matendo mema kwenye mabustani ya Pepo ambayo starehe yake ni ya daima, inapita mito chini ya miti yake, watapambwa humo kwa vidani vya dhahabu na kwa lulu; na nguo zao za kawaida Peponi ni hariri kwa wanawake na kwa wanaume.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net