Al-Hajj 22:22
الحجكُلَّمَآ أَرَادُوٓا۟ أَن يَخْرُجُوا۟ مِنْهَا مِنْ غَمٍّ أُعِيدُوا۟ فِيهَا وَذُوقُوا۟ عَذَابَ ٱلْحَرِيقِ
Kila wakitaka kutoka humo kwa sababu ya uchungu, watarudishwa humo humo, na wataambiwa: Onjeni adhabu ya kuunguza!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kila wakitaka kutoka humo kwa sababu ya uchungu watarudishwa humo humo, na wataambiwa: Onjeni adhabu ya kuungua! [22]
[22] Kila wakijaribu kutoka Motoni kwa wingi wa machungu na dhiki Malaika watawapiga nayo hayo marungu, na watarudishwa huko huko waliko kuwako. Na watawaambia: Onjeni adhabu ya Moto unao unguza kuwa ni malipo ya ukafiri wenu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kila wakijaribu kutoka Motoni, kwa sababu ya makero na mateso walionayo, watarudishwa adhabuni na wataambiwa, «Onjeni adhabu ya Moto unaochoma».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net