Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 22 · Aya ya 24

Al-Hajj 22:24

الحج

وَهُدُوٓا۟ إِلَى ٱلطَّيِّبِ مِنَ ٱلْقَوْلِ وَهُدُوٓا۟ إِلَىٰ صِرَٰطِ ٱلْحَمِيدِ

Maana

Na wataongozwa kwenye maneno mazuri, na wataongozwa kwenye njia ya Msifiwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wataongozwa kwenye maneno mazuri, na wataongozwa kwenye Njia ya Msifiwa. [24]

[24] Na ziada ya starehe yao humo Peponi ni kuwa Mwenyezi Mungu atawajaalia wawe na kauli njema, na vitendo vizuri vya kusifika. Basi watakuwa wakimtakasa Mwenyezi Mungu na kumtukuza, na watakuwa wenyewe kwa wenyewe wakiamiliana kwa mapenzi na amani.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwa hakika, Allah Mtukufu Aliwaongoza ulimwenguni kwenye neno zuri: tamshi la kumpwekesha Allah Mtukufu, kumshukuru na kumsifu, na huko Akhera wamshukuru Allah Mtukufu kwa mwisho mwema, kama vile Alivyowaongoza kabla ya hapo kufuata njia ya Uislamu inayosifiwa inayofikisha Peponi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hajj

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net