Al-Hajj 22:2
الحجيَوْمَ تَرَوْنَهَا تَذْهَلُ كُلُّ مُرْضِعَةٍ عَمَّآ أَرْضَعَتْ وَتَضَعُ كُلُّ ذَاتِ حَمْلٍ حَمْلَهَا وَتَرَى ٱلنَّاسَ سُكَـٰرَىٰ وَمَا هُم بِسُكَـٰرَىٰ وَلَـٰكِنَّ عَذَابَ ٱللَّهِ شَدِيدٌ
Siku mtakapoiona, kila mwenye kunyonyesha atamsahau amnyonyeshaye, na kila mwenye mimba, ataharibu mimba yake. Na utaona watu wamelewa, na kumbe hawakulewa. Lakini adhabu ya Mwenyezi Mungu ni kali.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Siku mtapo iona, kila mwenye kunyonyesha atamsahau amnyonyeshaye, na kila mwenye mimba ataharibu mimba yake. Na utaona watu wamelewa, na kumbe hawakulewa. Lakini adhabu ya Mwenyezi Mungu ni kali. [2]
[2] Siku mtapo kiona Kiyama mtaona kitisho chake kinafikilia ukubwa wake hata kama yupo mwanamke anaye nyonyesha na ziwa lake limo katika mdomo wa mwanawe, basi hapana shaka atamsahau na amwachilie mbali. Na kama yupo mwanamke ana mimba basi ataiharibu mimba kabla ya kufika wakati wake wa kuzaa kwa ajili ya fazaa na kitisho. Na ewe mwenye kuangalia! Ukiona hali ya watu Siku hiyo namna wanavyo onekana hawanazo, na wanapo kwenda wanayumba, utadhani wamelewa, na ilhali hawakulewa. Lakini kitisho walicho kishuhudia, na khofu ya adhabu kuu ya Mwenyezi Mungu ndiyo iliyo waondoshea utulivu wao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Siku mtakapokiona Kiyama kimesima, mama atamsahau mtoto wake mchanga aliyempa titi lake kunyonya kwa shida iliyomshukia, mwenye mimba ataharibu mimba yake kwa babaiko, na akili za watu zitapotea, watakuwa ni kama walevi kwa tukio hilo kubwa na babaiko, na hali wao si walevi wa pombe, lakini ni ukali wa adhabu ndio uliowapoteza akili zao na hisia zao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net