Al-Hajj 22:1
الحجيَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ٱتَّقُوا۟ رَبَّكُمْ ۚ إِنَّ زَلْزَلَةَ ٱلسَّاعَةِ شَىْءٌ عَظِيمٌ
Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi. Hakika mtetemeko wa Saa (ya Kiyama) ni jambo kuu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi. Hakika tetemeko la Saa (ya Kiyama) ni jambo kuu. [1]
[1] Enyi watu! Tahadharini na adhabu ya Mola wenu Mlezi, na wekeni katika nyoyo zenu makumbusho ya Siku ya Kiyama. Kwani mtingishiko utao tokea hapo ni mkubwa, wenye kuhangaisha na kutikisa viumbe.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi watu! Tahadharini na mateso ya Allah Mtukufu, kwa kufuata amri zake na kuepuka makatazo yake, kwani vitisho vitakavyotokea pindi kisimamapo Kiyama na mtetemeko mkubwa wa ardhi utakaofanya pembe zake zipasukepasuke, ni jambo kubwa ambalo hakuna mwenye kulikadiria wala kulifikia vile litakavyokuwa, wala kujua namna yake isipokua Mola wa viumbe wote.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net