Al-Anbiyaa 21:112
الأنبياءقَـٰلَ رَبِّ ٱحْكُم بِٱلْحَقِّ ۗ وَرَبُّنَا ٱلرَّحْمَـٰنُ ٱلْمُسْتَعَانُ عَلَىٰ مَا تَصِفُونَ
Sema: Mola wangu Mlezi! Hukumu kwa haki. Na Mola wetu Mlezi ndiye Mwingi wa rehema, aombwaye msaada juu ya mnayoyazua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Mola wangu Mlezi! Hukumu kwa haki. Na Mola wetu Mlezi ni Mwingi wa Rehema, aombwaye msaada juu ya mnayo yazua;. [112]
[112] Ewe Nabii! Sema: Ewe Mola Mlezi! Tuhukumu baina yangu na hawa nilio wafikishia Wahyi kwa uadilifu ili wasiwe sawa Waumini na makafiri. Na Mola wetu Mlezi Mwenye kuneemesha kwa neema kubwa, Mwenye kustahiki kuhimidiwa na kushukuriwa, ndiye wa kutakiwa msaada kuvunja uzushi mnao zua, enyi makafiri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Nabii, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukiye, akasema, Mola wangu! Amua baina yetu na watu wetu walioukanusha Uamuzi wa haki, na tunamuomba Mola wetu Mwingi wa rehema, tunataka msaada Wake tuzibatilishe sifa mnazombandika, enyi makafiri, za ushirikina na ukanushaji na uzushi na juu ya maonyo mnayotuonya kuwa mtakuwa na nguvu na ushindi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net