Al-Hajj 22:18
الحجأَلَمْ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ يَسْجُدُ لَهُۥ مَن فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَن فِى ٱلْأَرْضِ وَٱلشَّمْسُ وَٱلْقَمَرُ وَٱلنُّجُومُ وَٱلْجِبَالُ وَٱلشَّجَرُ وَٱلدَّوَآبُّ وَكَثِيرٌ مِّنَ ٱلنَّاسِ ۖ وَكَثِيرٌ حَقَّ عَلَيْهِ ٱلْعَذَابُ ۗ وَمَن يُهِنِ ٱللَّهُ فَمَا لَهُۥ مِن مُّكْرِمٍ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ يَفْعَلُ مَا يَشَآءُ ۩
Je! Huoni kwamba vinamsujudia Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini, na jua, na mwezi, na nyota, na milima, na miti, na wanyama, na wengi miongoni mwa watu. Na wengi imewastahiki adhabu. Na anayefedheheshwa na Mwenyezi Mungu, huyo hana wa kumheshimu. Hakika Mwenyezi Mungu hutenda atakavyo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je! Huoni kwamba vinamsujudia Mwenyezi Mungu viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi, na jua, na mwezi, na nyota, na milima, na miti, na wanyama, na wengi miongoni mwa watu. Na wengi imewastahiki adhabu. Na anaye fedheheshwa na Mwenyezi Mungu hana wa kumhishimu. Hakika Mwenyezi Mungu hutenda apendayo. [18]
[18] Ewe mwenye akili! Hujui kwamba hakika Mwenyezi Mungu vinamnyenyekea na kumt'ii vyote viliomo mbinguni na katika ardhi, na jua, na mwezi, na nyota, na milima, na miti, na wanyama, na wengi katika watu wanamuamini Mwenyezi Mungu na wanafuata maamrisho yake, na kwa hivyo wanastahiki Pepo? Na wapo wengi miongoni mwao wanao puuza na wala hawamuamini, wala hawayatendi maamrisho yake, na kwa hivyo wanastahiki adhabu na hizaya. Na anaye fukuzwa na Mwenyezi Mungu kutokana na rehema yake basi hawezi yeyote kumhishimu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu. Kwani Yeye hutenda ayapendayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Je hujui, ewe Mtume, kwamba Allah Mtukufu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, wanamsujudia Yeye, katika hali ya kunyenyekea na kufuata amri, Malaika walioko mbinguni, viumbe walioko ardhini, jua, mwezi, majabali, miti na wanyama? Na wanamsujudia Allah Mtukufu, kwa kutii na kwa hiari, watu wengi, nao ni Waumini. Na kuna watu wengi imepasa adhabu juu yao, na kwa hivyo wao ni watwevu. Na yoyote yule ambaye Allah Mtukufu Amemtweza hakuna yoyote wa kumtukuza. Hakika Allah Mtukufu Anafanya kwa viumbe vyake Atakalo kuambatana na hekima Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net