Al-Hajj 22:19
الحجهَـٰذَانِ خَصْمَانِ ٱخْتَصَمُوا۟ فِى رَبِّهِمْ ۖ فَٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ قُطِّعَتْ لَهُمْ ثِيَابٌ مِّن نَّارٍ يُصَبُّ مِن فَوْقِ رُءُوسِهِمُ ٱلْحَمِيمُ
Hawa ni wagomvi wawili waliogombana kwa ajili ya Mola wao Mlezi. Basi waliokufuru watakatiwa nguo za moto, na yatamiminwa juu ya vichwa vyao maji yanayochemka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hawa wagomvi wawili walio gombana kwa ajili ya Mola wao Mlezi. Basi walio kufuru watakatiwa nguo za moto, na yatamiminwa juu ya vichwa vyao maji yanayo chemka. [19]
[19] Haya ni makundi mawili walio zozana kwa mambo yaliyo mkhusu Mola wao Mlezi, na yanayo mstahiki na yasio mstahiki. Kikundi kimoja kikamuamini na kikundi kingine kikakataa. Basi wale walio kataa na kukufuru Mwenyezi Mungu amewaandalia Siku ya Kiyama moto utao wazunguka na kuwapamba kila upande, kama nguo inavyo upamba mwili. Na kuzidi kuwaadhibu Malaika watawamiminia maji ya moto mno juu ya vichwa vyao!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Haya ni mapote mawili ya watu, wametafautiana kuhusu Mola wao: watu wa Imani na watu wa ukafiri, kila mmoja anadai kuwa yeye yuko kwenye usawa. Wale waliokufuru watazungukwa na adhabu yenye sura ya nguo za Moto walizopatiwa wazivae, zitaichoma miili yao na yatamiminwa juu ya vichwa vyao maji yaliyofikia upeo wa ukali,
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net