Al-Hajj 22:17
الحجإِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَٱلَّذِينَ هَادُوا۟ وَٱلصَّـٰبِـِٔينَ وَٱلنَّصَـٰرَىٰ وَٱلْمَجُوسَ وَٱلَّذِينَ أَشْرَكُوٓا۟ إِنَّ ٱللَّهَ يَفْصِلُ بَيْنَهُمْ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ شَهِيدٌ
Hakika walioamini, na Mayahudi na Wasabai na Wakristo na Majusi na wale walioshirikisha, hakika Mwenyezi Mungu atawapambanua baina yao Siku ya Kiyama. Hakika Mwenyezi Mungu ni Shahidi wa kila kitu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika walio amini, na ambao ni Mayahudi na Wasabai na Wakristo na Majusi na wale walio shiriki - hakika Mwenyezi Mungu atawapambanua baina yao Siku ya Kiyama. Hakika Mwenyezi Mungu ni Shahidi wa kila kitu. [17]
[17] Hakika wanao muamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake wote, na Mayahudi wanao nasibika na Musa, na waabuduo nyota na Malaika, na Wakristo wanao nasibika na Isa, na Majusi wanao abudu moto, na washirikina wanao abudu masanamu..hakika wote hawa Mwenyezi Mungu atakuja wapambanua mbali mbali Siku ya Kiyama kwa kumdhihirisha mwenye haki na aliye potea kati yao. Kwani Yeye anajua vyema vitendo vyote vya viumbe vyake. Na atawalipa kwa vitendo vyao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika wale waliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na Mayahudi na Sâbiûn (watu waliobaki kwenye maumbile yao na hawana dini wanayoifuata) na Wanaswara na Majûs (wanaoabudu moto) na wale walioshirikisha (wanaoabudu masanamu), Allah Mtukufu Atapambanua baina yao wote, Siku ya Kiyama, Awatie Waumini Peponi na Awatie makafiri Motoni, Allah Mtukufu juu ya kila kitu ni Shahidi, Anayashuhudia matendo yote ya waja, Anayadhibiti na Anayahifadhi, Na Atamlipa kila mtu kile anachostahili, malipo yanayolingana na matendo waliokuwa wakiyafanya.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net