Al-Hajj 22:16
الحجوَكَذَٰلِكَ أَنزَلْنَـٰهُ ءَايَـٰتٍۭ بَيِّنَـٰتٍ وَأَنَّ ٱللَّهَ يَهْدِى مَن يُرِيدُ
Na namna hivyo tumeiteremsha (Qur-ani) kuwa ni Aya zilizo wazi, na hakika Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na namna hivi tumeiteremsha (Qur'ani) kuwa ni Aya zilizo wazi, na hakika Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye. [16]
[16] Mfano wa tulivyo bainisha hoja zetu zi wazi katika tuliyo kwisha wateremshia Mitume. Tumemteremshia Muhammad Qur'ani yote, nayo ni Aya zilizo wazi ili ziwe ni hoja juu ya watu. Na hakika Mwenyezi Mungu humuongoa amtakaye kuwaongoa ili isalimike tabia yake na abaidike mbali na inadi na yanayo sabibisha hayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kama Alivyosimamisha Allah Mtukufu hoja, miongoni mwa dalili za uwezo Wake, juu ya makafiri kuhusu ufufuzi, vilevile Aliiteremsha Qur’ani, ambayo aya zake ziko wazi katika matamshi yake na maana yake, na ambayo kwayo Allah Mtukufu Anamuongoza anayemtaka aongoke. Kwani hakuna Mwenye kuongoa isipokuwa Yeye.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net