Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 22 · Aya ya 15

Al-Hajj 22:15

الحج

مَن كَانَ يَظُنُّ أَن لَّن يَنصُرَهُ ٱللَّهُ فِى ٱلدُّنْيَا وَٱلْـَٔاخِرَةِ فَلْيَمْدُدْ بِسَبَبٍ إِلَى ٱلسَّمَآءِ ثُمَّ لْيَقْطَعْ فَلْيَنظُرْ هَلْ يُذْهِبَنَّ كَيْدُهُۥ مَا يَغِيظُ

Maana

Anayedhani kwamba Mwenyezi Mungu hatamnusuru (Mtume) katika dunia na Akhera, basi na afunge kamba kwenye dari kisha na aikate, na atazame je hila yake itayaondoa hayo yaliyomkasirisha?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Anaye dhani kwamba Mwenyezi Mungu hatamnusuru (Mtume) katika dunia na Akhera na afunge kamba kwenye dari kisha aikate. Atazame je hila yake itaondoa hayo yaliyo mkasirisha? [15]

[15] Ikiwa miongoni mwa makafiri yupo anaye dhani kwamba Mwenyezi Mungu hatamsaidia Nabii wake, basi na anyooshe kamba mpaka kwenye dari ya nyumba yake. Kisha ajinyonge, na akadirie katika nafsi yake na atazame, je, kitendo chake hicho kitaondoa hayo yanayo muudhi ya kuwa Mwenyezi Mungu anamnusuru Mtume wake?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Yoyote yule anayeitakidi kwamba Allah Mtukufu Aliyetukuka hatamsaidia Mtume Wake kwa kumpa ushindi ulimwenguni kwa kuipa nguvu Dini yake na huko Akhera kumtukuza daraja yake na kumuadhibu aliyemkanusha, basi anyoshe kamba aifunge kwenye sakafu ya nyumba yake kisha ajitie kitanzi kisha aikate hiyo kamba, kisha aangalie iwapo hilo litamuondolea hasira alizonazo ndani ya nafsi yake. Allah Mtukufu ni Mwenye kumnusuru Nabii Wake Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), hapana budi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hajj

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net