Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 22 · Aya ya 14

Al-Hajj 22:14

الحج

إِنَّ ٱللَّهَ يُدْخِلُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ جَنَّـٰتٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ يَفْعَلُ مَا يُرِيدُ

Maana

Hakika Mwenyezi Mungu atawaingiza wale walioamini na wakatenda mema katika Bustani zipitazo mito kwa chini yake. Hakika Mwenyezi Mungu hutenda atakayo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika Mwenyezi Mungu atawaingiza walio amini na wakatenda mema katika Bustani zipitazo mito kati yake. Hakika Mwenyezi Mungu hutenda atakayo. [14]

[14] Hakika wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake kwa Imani yenye kuambatana na vitendo vyema, Mola wao Mlezi atawatia Siku ya Kiyama katika Bustani zipitwazo chini ya miti yake na mito. Hakika Mwenyezi Mungu hutenda apendavyo kumuadhibu mharibifu na kumlipa mema mtenda mema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika Allah Mtukufu Atawatia, wale ambao walimuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na wakajikita katika hiyo Imani na wakafanya mema, kwenye mabustani ya Pepo ambayo inapita mito chini ya majumba yake ya fahari na miti yake. Hakika Allah Mtukufu Anafanya Analolitaka la kuwapa malipo mazuri wenye kumtii kwa ukarimu, Wake na kuwatesa wenye kumuasi kwa uadilifu Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hajj

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net