Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 99

Al-Anbiyaa 21:99

الأنبياء

لَوْ كَانَ هَـٰٓؤُلَآءِ ءَالِهَةً مَّا وَرَدُوهَا ۖ وَكُلٌّ فِيهَا خَـٰلِدُونَ

Maana

Lau kuwa hawa ni miungu, wasingelingia humo. Na wote watadumu humo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Lau kuwa hawa ni miungu, wasingeli ingia. Na wote watadumu humo. [99]

[99] Lau kama hawa mlio waabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni miungu inayo stahiki kuabudiwa, wasingeli ingia nanyi humo. Na nyote, wenye kuabudu na kuabudiwa, mtabaki Motoni, wala hamtatoka.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Lau hawa ambao mliwaabudu badala ya Allah Mtukufu Aliyetukuka wangekua ni waungu wanaostahiki kuabudiwa, wasingeingia moto wa Jahanamu pamoja na nyinyi, enyi washirikina. Kwa hakika, wote hao, waabudu na waabudiwa, ni wenye kukaa milele ndani ya moto wa Jahanamu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net