Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 98

Al-Anbiyaa 21:98

الأنبياء

إِنَّكُمْ وَمَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ حَصَبُ جَهَنَّمَ أَنتُمْ لَهَا وَٰرِدُونَ

Maana

Hakika nyinyi na hao mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni kuni za Jahannamu; huko mtaingia tu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika nyinyi na hao mnao waabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni kuni za Jahannamu; huko mtaingia tu. [98]

[98] Wataambiwa makafiri hawa: Nyinyi na hiyo miungu mliyo kuwa mkiiabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni kuni za Moto wa Jahannamu. Nyinyi mtaingia humo muadhibiwe!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwa hakika, nyinyi, enyi makafiri, na vitu ambavyo mlikuwa mkiviabudu badala ya Allah Mtukufu, miongoni mwa masanamu, na wale walioridhia muwaabudu, kati ya majini na binadmu, ni viwashio vya moto wa Jahanamu na ni kuni zake, nyinyi na wao humo mtaingia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net