Al-Anbiyaa 21:97
الأنبياءوَٱقْتَرَبَ ٱلْوَعْدُ ٱلْحَقُّ فَإِذَا هِىَ شَـٰخِصَةٌ أَبْصَـٰرُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ يَـٰوَيْلَنَا قَدْ كُنَّا فِى غَفْلَةٍ مِّنْ هَـٰذَا بَلْ كُنَّا ظَـٰلِمِينَ
Na Miadi ya haki ikakaribia. Hapo ndipo yatakapokodoka macho ya waliokufuru (na watasema): Ole wetu! Bila ya shaka tulikuwa tumeghafilika mbali na haya, bali tulikuwa wenye kudhulumu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na miadi ya haki ikakaribia. Hapo ndipo yatapo kodoka macho ya walio kufuru (na watasema:) Ole wetu! Bila ya shaka tulikuwa tumeghafilika na haya, bali tulikuwa wenye kudhulumu. [97]
[97] Na ikakaribia miadi iliyo haina budi kutimizwa, nayo ni Siku ya Kiyama, wakawa wale walio kufuru wanakutikana wakikodoa macho yao kwa wingi wa kitisho, wakipiga makelele kusema: Kitisho gani hichi cha kutuangamiza! Hakika sisi tulighafilika na Siku hii. Bali tulikuwa ni wenye kujidhulumu nafsi zetu kwa ukafiri na inda.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
hapo Siku ya Kiyama itakuwa imekaribia na matukio yake yatajitokeza, na hapo utayaona macho ya makafiri yamekodoka hayapepesi kwa kibabaiko kikali, huku wakiwa wanajiapiza maangamivu kwa majuto wakisema, «Ee ole wetu! Kwa hakika tulikuwa tumeghafilika na Siku hii na kujiandalia nayo na kwa hivyo tulikuwa madhalimu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net