Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 96

Al-Anbiyaa 21:96

الأنبياء

حَتَّىٰٓ إِذَا فُتِحَتْ يَأْجُوجُ وَمَأْجُوجُ وَهُم مِّن كُلِّ حَدَبٍ يَنسِلُونَ

Maana

Mpaka watakapofunguliwa Yaajuju na Maajuju wakawa wanateremka haraka kutoka kwenye kila kilima.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mpaka watapo funguliwa Juju na Maajuju wakawa wanateremka kutoka kila mlima; [96]

[96] Mpaka itapo funguliwa milango ya shari na ufisadi, wakaingia wana wa Juju na Maajuju wakikimbizana kuteremka milimani na majiani kwa kufanya vitendo vya fujo na rabsha.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi pindi kitakapofunguliwa kizuizi cha Ya’jûj na Ma’jûj, na wakatoka kwenye ardhi za juu wakaenea kwenye pande zake kwa haraka.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net