Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 95

Al-Anbiyaa 21:95

الأنبياء

وَحَرَٰمٌ عَلَىٰ قَرْيَةٍ أَهْلَكْنَـٰهَآ أَنَّهُمْ لَا يَرْجِعُونَ

Maana

Na haiwi kwa wana mji tuliouangamiza, ya kwamba hawatarejea.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na haiwi kwa wana-mji tulio uangamiza, ya kwamba hawatarejea, [95]

[95] Na haitakuwa kwa watu wa mji tulio uteketeza kwa sababu ya dhulma yao kwamba hawatarejea kwetu Siku ya Kiyama, bali hapana budi kuwa watarejea na tutawahisabia vitendo vyao viovu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Haiwezekani kwa watu wa miji tuliyoiangamiza, kwa sababu ya ukanushaji wao na dhulma zao, kurudi duniani kabla ya Siku ya Kiyama ili kurekebisha kasoro zao ambazo walikuwa nazo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net