Al-Anbiyaa 21:94
الأنبياءفَمَن يَعْمَلْ مِنَ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَا كُفْرَانَ لِسَعْيِهِۦ وَإِنَّا لَهُۥ كَـٰتِبُونَ
Na atendaye mema naye ni Muumini, basi haitakataliwa juhudi yake. Na hakika Sisi tunamwandikia.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na atendaye mema naye ni Muumini basi haitakataliwa juhudi yake. Na hakika Sisi tunamwandikia. [94]
[94] Basi mwenye kutenda vitendo vyake vyema, naye ni mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Dini yake aliyo iridhia, hatopunguziwa kitu katika juhudi yake. Bali atalipwa malipo kaamili. Na Sisi ni wenye kuiandika hiyo juhudi yake. Basi hakitopotea kitu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi Mwenye kujilazimisha kumuamini Allah Mtukufu na Mitume Wake na akafanya awezayo ya matendo mema kwa kumtii Allah Mtukufu na kumuabudu, Allah Mtukufu Hayapotezi matendo Yake wala Hayabatilishi, bali Anayaongeza yote hayo mara dufu, na atayakuta aliyoyatenda kwenye Kitabu chake siku atakayofufuliwa baada ya kufa kwake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net