Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 93

Al-Anbiyaa 21:93

الأنبياء

وَتَقَطَّعُوٓا۟ أَمْرَهُم بَيْنَهُمْ ۖ كُلٌّ إِلَيْنَا رَٰجِعُونَ

Maana

Nao wakalikata jambo lao hili mapande mapande baina yao. Wote watarudi kwetu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Nao wakalikata jambo lao hili mapande mapande baina yao. Wote watarudi kwetu. [93]

[93] Na juu ya kuwepo uwongozi huu aghlabu ya watu wamegawanyika kwa mujibu wa matamanio yao, wakafanya mambo yao ya Dini mapande mapande, wakawa makundi mbali mbali. Na kila kundi litaturejea Sisi tulihisabie vitendo vyake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Lakini watu walitafautiana juu ya Mitume wao, na wengi wa wafauasi wao katika dini walifarikiana wakawa ni makundi na mapote, wakaabudu viumbe na matamanio. Na wote hao ni wenye kurejea kwetu na ni wenye kuhesabiwa juu ya yale waliyoyafanya.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net