Al-Anbiyaa 21:92
الأنبياءإِنَّ هَـٰذِهِۦٓ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَٰحِدَةً وَأَنَا۠ رَبُّكُمْ فَٱعْبُدُونِ
Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo niabuduni Mimi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo niabuduni Mimi. [92]
[92] Hakika mila hii, nayo ndiyo Uislamu, ndiyo mila iliyo sahihi inayo kupasini kuilinda, kwa kuwa ni mila moja iliyo shikamana wala haikukhitalifiana baina ya hukumu zake. Basi nanyi msifarikiene katika mila hii kwa makundi na vyama. Na Mimi ndiye Muumba wenu, na Mwenye kumiliki mambo yenu yote. Basi niabuduni Mimi tu, wala msinishirikishe na mwengine.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Manabii hawa wote, dini yao ni moja, nayo ni Uislamu. Nao ni kujisalimisha kwa Allah Mtukufu kwa kuwa mtiifu na kumpwekesha Yeye kwa ibada. Na Allah Mtukufu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Ndiye Bwana wa viumbe, basi muabuduni, enyi watu, Peke Yake, Asiye na mshirika.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net