Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 91

Al-Anbiyaa 21:91

الأنبياء

وَٱلَّتِىٓ أَحْصَنَتْ فَرْجَهَا فَنَفَخْنَا فِيهَا مِن رُّوحِنَا وَجَعَلْنَـٰهَا وَٱبْنَهَآ ءَايَةً لِّلْعَـٰلَمِينَ

Maana

Na yule mwanamke aliyeulinda uke wake, na tukampulizia katika roho yetu, na tukamfanya yeye na mwanawe kuwa ni Ishara kwa walimwengu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na mwanamke aliye linda uke wake, na tukampulizia katika roho yetu, na tukamfanya yeye na mwanawe kuwa ni Ishara kwa walimwengu. [91]

[91] Pamoja na hawa simulia kisa cha Maryamu aliye ulinda uke wake, nasi tukamfikishia siri katika siri zetu. Tukamjaalia achukue mimba bila ya mume, na tukamjaalia mwanawe azaliwe bila ya baba. Akawa yeye na mwanawe dalili iliyo wazi ya uweza wetu kugeuza sababu na vinavyo sabibishwa. Na hakika Sisi ni waweza wa kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kumbuka, ewe Mtume, kisa cha Maryam binti ya ‛Imrân aliyeihifadhi tupu yake na haramu na asifanye uzinifu katika maisha yake. Allah Mtukufu Akamtuma Jibrili, amani imshukie, kwake akapuliza katika mfuko wa kanzu yake, na ule mpulizo ukafika kwenye kizazi chake, na Allah Mtukufu akamuumba Al-Masĩḫ ‘Ǐsâ, amani imshukie. Hivyo basi akabeba mimba yake bila ya mume, na kwa ajili hiyo akawa, yeye na mwanawe, ni alama ya uwezo wa Allah Mtukufu na mazingatio kwa viumbe mpaka kusimama Kiyama.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net