Al-Anbiyaa 21:100
الأنبياءلَهُمْ فِيهَا زَفِيرٌ وَهُمْ فِيهَا لَا يَسْمَعُونَ
Lao wao humo ni kupiga mayowe, na wala hawatasikia (jinginelo).
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Lao wao humo ni kupiga mayowe, na wala hawatasikia (jenginelo). [100]
[100] Humo watatoa pumzi zitokazo vifuani kwa sauti kama ya mwenye kukabwa, kwa dhiki watayo pata, na hawatasikia la kuwafurahisha.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hawa wenye kuadhibiwa Motoni wataona uchungu unaooneshwa na mlio wa sauti zao ambapo pumzi zao zinatoka kwa nguvu sana kutoka kwenye vifua vyao. Na wao wakiwa Motoni hawasikii kwa ukali wa adhabu wanayopewa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net