Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 101

Al-Anbiyaa 21:101

الأنبياء

إِنَّ ٱلَّذِينَ سَبَقَتْ لَهُم مِّنَّا ٱلْحُسْنَىٰٓ أُو۟لَـٰٓئِكَ عَنْهَا مُبْعَدُونَ

Maana

Ama wale ambao wema wetu umewatangulia, hao watatenganishwa na hayo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ama wale ambao wema wetu umewatangulia, hao watatenganishwa na hayo. [101]

[101] Hakika wale tulio wakubalia kwa kufuata kwao Haki na vitendo vya kheri, na tukawaahidi malipo mema, hao watawekwa mbali kabisa na Jahannamu na adhabu yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwa hakika, wale ambao kimetangulia kwetu sisi kitangulizi chema katika ujuzi wetu kuwa watakuwa ni watu wa Peponi, hao wataepushwa na Moto, hawatauingia wala hawatakuwa karibu nao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net