Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 86

Al-Anbiyaa 21:86

الأنبياء

وَأَدْخَلْنَـٰهُمْ فِى رَحْمَتِنَآ ۖ إِنَّهُم مِّنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ

Maana

Na tukawaingiza katika rehema yetu. Hakika wao walikuwa katika watu wema.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tukawaingiza katika rehema yetu. Hakika wao walikuwa katika watu wema. [86]

[86] Na tukawajaalia miongoni mwa watu wa kupata rehema yetu. Hakika hao ni katika waja wetu wema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na tukawatia ndani ya rehema zetu. Kwa hakika wao ni miongoni mwa wale ambao imetengenea ndani yao na nje yao, wakamtii Allah Mtukufu na wakafanya matendo yanayolingana na maamrisho Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net