Al-Anbiyaa 21:85
الأنبياءوَإِسْمَـٰعِيلَ وَإِدْرِيسَ وَذَا ٱلْكِفْلِ ۖ كُلٌّ مِّنَ ٱلصَّـٰبِرِينَ
Na Ismail, na Idris, na Dhulkifli, wote walikuwa miongoni mwa wanaosubiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Ismail, na Idris, na Dhulkifli - wote walikuwa miongoni mwa wanao subiri. [85]
[85] Ewe Nabii! Watajie watu wako khabari za Ismail, na Idris, na Dhulkifli. Wote hao ni miongoni wanao subiri wakahimili taklifa na shida.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kumbuka Ismâ‛ĩl, Idrĩs na Dhulkifl. Wote hao ni miongoni mwa wavumilivu katika kumtii Allah Mtukufu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, katika kujiepusha na kumuasi na juu ya makadirio Yake, na kwa hivyo walistahiki kutajwa kwa sifa nzuri.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net