Al-Anbiyaa 21:84
الأنبياءفَٱسْتَجَبْنَا لَهُۥ فَكَشَفْنَا مَا بِهِۦ مِن ضُرٍّ ۖ وَءَاتَيْنَـٰهُ أَهْلَهُۥ وَمِثْلَهُم مَّعَهُمْ رَحْمَةً مِّنْ عِندِنَا وَذِكْرَىٰ لِلْعَـٰبِدِينَ
Basi tukamwitikia, na tukamwondolea madhara aliyokuwa nayo, na tukampa watu wake na mfano wao pamoja nao kuwa ni rehema inayotoka kwetu, na ukumbusho kwa wafanyao ibada.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi tukamwitikia, na tukamwondolea madhara aliyo kuwa nayo, na tukampa watu wake na mfano wao pamoja nao kuwa ni rehema inayo toka kwetu, na ukumbusho kwa wafanyao ibada. [84]
[84] Tukamwitikia kwa aliyo yaomba, tukamwondolea madhara, na tukampa watoto kwa kadri ya waliyo kwisha kufa. Na tukamwongezea mfano wa wale, kuwa ni rehema iliyo tokana na fadhila yetu, na pia ni kuwa ni kumbusho kwa wenginewe wanao tuabudu ili wapate nao kusubiri kama alivyo subiri yeye, na watumai kupata rehema ya Mwenyezi Mungu kama alivyo tumai yeye.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hapo tukayakubali maombi yake, tukamuondolea matatizo na tukamrudishia alichokikosa miongoni mwa wake, watoto na mali mara mbili zaidi. Tulimfanyia hayo kwa huruma itokayo kwetu na ili awe ni kiigizo kwa kila mwenye kuvumilia mitihani, mwenye matumaini ya kupata rehema za Mola wake na mwenye kumuabudu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net