Al-Anbiyaa 21:83
الأنبياءوَأَيُّوبَ إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُۥٓ أَنِّى مَسَّنِىَ ٱلضُّرُّ وَأَنتَ أَرْحَمُ ٱلرَّٰحِمِينَ
Na Ayyubu, alipomwita Mola wake Mlezi, akasema: Mimi yamenipata madhara. Na Wewe ndiye unayerehemu kuliko wote wanaorehemu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Ayyubu, alipo mwita Mola wake Mlezi, akasema: Mimi yamenipata madhara. Na Wewe ndiye unaye rehemu kuliko wote wanao rehemu. [83]
[83] Ewe Nabii! Mtaje Ayyubu, pale alipo mwita Mola wake Mlezi, na maradhi yalikwisha mdhoofisha, na akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika nimesibiwa na madhara na yananiuma! Na Wewe ni Mbora wa wanao rehemu..
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kumbuka, ewe Mtume, mja wetu Ayyûb, tulipomtahini kwa madhara na ugonjwa mkubwa mwilini mwake, na akakosa watu wake, mali yake na watoto wake, akasubiri kwa kutaka thawabu, na akamlingania Mola wake, Aliyetukuka na kushinda, kwa kumuomba, «Mimi nimepatikana na madhara, na wewe Ndiye Mwenye huruma kuliko wenye huruma, basi niepushie nayo!»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net