Al-Anbiyaa 21:82
الأنبياءوَمِنَ ٱلشَّيَـٰطِينِ مَن يَغُوصُونَ لَهُۥ وَيَعْمَلُونَ عَمَلًا دُونَ ذَٰلِكَ ۖ وَكُنَّا لَهُمْ حَـٰفِظِينَ
Na pia mashetani wanaompigia mbizi na kufanya kazi nyenginezo. Na Sisi tulikuwa walinzi wao.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na pia mashet'ani wanao mpigia mbizi na kufanya kazi nyenginezo. Na Sisi tulikuwa walinzi wao. [82]
[82] Na tukawafanya mashetani wamtumikie kwa kuzamia chini baharini kumletea lulu na marijani; na wakifanya kazi nyenginezo, kama kujenga ngome na majumba ya kifalme. Na Sisi tulikuwa tukiwaangalia katika kazi zao hizo, basi hapana hata mmoja wao aliye pata shida, wala hawakuvunja amri ya Suleiman.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tulimdhalilishia Sulaymân, kati ya mashetani, mashetani ambao alikuwa akiwatuma kufanya yale ambayo wasiokuwa wao wanashindwa nayo, walikuwa wakipiga mbizi baharini wakimtolea lulu na johari, na walikuwa wakimtengenezea vitu avitakavyo kwao, hawakuwa wakiweza kukataa kufanya ayatakayo kutoka kwao. Allah Mtukufu Amewahifadhi kwa nguvu Zake kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net