Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 81

Al-Anbiyaa 21:81

الأنبياء

وَلِسُلَيْمَـٰنَ ٱلرِّيحَ عَاصِفَةً تَجْرِى بِأَمْرِهِۦٓ إِلَى ٱلْأَرْضِ ٱلَّتِى بَـٰرَكْنَا فِيهَا ۚ وَكُنَّا بِكُلِّ شَىْءٍ عَـٰلِمِينَ

Maana

Na tukamsahilishia Suleiman upepo wa kimbunga uendao kwa amri yake kwenye ardhi tuliyoibariki. Na Sisi ndio tunaojua kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tukamsahilishia Suleiman upepo wa kimbunga wendao kwa amri yake kwenye ardhi tuliyo ibarikia. Na Sisi ndio tunao jua kila kitu. [81]

[81] Na tulimsahilishia Suleiman upepo unao vuma kwa nguvu umtumikie, nao huo ulikuwa unakwenda kwa kufuata amri yake mpaka kwenye nchi tuliyo izidishia kheri yake. Nasi ni wenye kuyajua yote hayo. Halitupotei kubwa wala dogo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na tulimdhalilishia Sulaymân upepo wenye kuvuma kwa kasi ukimchukua yeye na walio pamoja naye, ukawa unapita kwa amri yake kuelekea ardhi ya Bayt al-Maqdis iliyoko Shâm ambayo tuliibariki kwa kheri nyingi. Na ujuzi wetu umeenea vitu vyote.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net