Al-Anbiyaa 21:87
الأنبياءوَذَا ٱلنُّونِ إِذ ذَّهَبَ مُغَـٰضِبًا فَظَنَّ أَن لَّن نَّقْدِرَ عَلَيْهِ فَنَادَىٰ فِى ٱلظُّلُمَـٰتِ أَن لَّآ إِلَـٰهَ إِلَّآ أَنتَ سُبْحَـٰنَكَ إِنِّى كُنتُ مِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ
Na Dhun-Nun alipoondoka hali ameghadhabika, na akadhani ya kwamba hatutamtia dhikini. Basi aliita katika giza: Hakuna mungu isipokuwa Wewe Subhanaka (Uliyetakasika). Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Dhun-Nun alipoondoka hali ameghadhibika, na akadhani ya kwamba hatutakuwa na uwezo juu yake. Basi aliita katika giza: Hapana mungu isipo kuwa Wewe Subhanaka Uliye takasika. Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu. [87]
[87] Ewe Nabii! Taja kisa cha Yunus, aliye mezwa na samaki..Pale alipoona dhiki kwa vile watu wake walipo puuza wito wake, naye akawahama akenda mbali nao na huku amewakasirikia. Akadhani ya kuwa Mwenyezi Mungu amemruhusu kuwahama, na kwamba haitopita hukumu juu yake. Samaki akammeza, na akaishi katika kiza cha bahari. Akamwita Mola wake Mlezi kwa kumnyenyekea, na kuungama aliyo kuwa nayo, akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Hapana wa kuabudiwa kwa haki ila Wewe. Ninakutakasa na kila lisio kuelekea Wewe. Ninaungama kuwa hakika mimi nilikuwa miongoni mwa walio dhulumu nafsi zao kwa kutenda yasio kupendeza.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kumbuka kisa cha mtu wa chewa, naye ni Yûnus mtoto wa Mattâ, (amani imshukie), Allah Mtukufu alimtuma kwa watu wake, akawalingania wakakataa kumuamini, akawaonya kuwa wataadhibiwa, lakini hawakurudi nyuma. Na akaachana nao bila kuwavumilia kama vile Allah Mtukufu Alivyomuamrisha, na akaondoka kutoka kwao akiwa na hasira juu yao, akiwa amebanwa na kifua kwa kuasi kwao. Na akadhani kwamba Allah Mtukufu Hatampa dhiki na kumuadhibu kwa ukiukaji huu. Allah Mtukufu Akamtahini kwa dhiki nyingi na kifungo na akamezwa na chewa baharini, na akamuita Mola wake kwa kumuomba katika giza la usiku, akiwa kwenye bahari na tumbo la chewa, hali ya kutubia na kukubali ukiukaji wake kwa kuacha kuwavumilia watu wake, huku akisema, «Hapana muabudiwa kwa haki isipokuwa wewe! Kutakasika na sifa za upungufu ni kwako! kwa hakika mimi nimekuwa miongoni mwa wenye kudhulumu!»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net