Al-Anbiyaa 21:78
الأنبياءوَدَاوُۥدَ وَسُلَيْمَـٰنَ إِذْ يَحْكُمَانِ فِى ٱلْحَرْثِ إِذْ نَفَشَتْ فِيهِ غَنَمُ ٱلْقَوْمِ وَكُنَّا لِحُكْمِهِمْ شَـٰهِدِينَ
Na Daud na Suleiman walipokata hukumu katika suala la konde walipolisha humo mbuzi wa watu usiku. Na Sisi tulikuwa wenye kushuhudia hukumu yao hiyo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Daud na Suleiman walipo kata hukumu katika kadhiya ya konde walipo lisha humo mbuzi wa watu usiku. Na Sisi tulikuwa wenye kushuhudia hukumu yao hiyo. [78]
[78] Ewe Nabii! Wataje Daud na Suleiman walipo toa hukumu katika kesi ya konde, ilio ingiliwa na mbuzi wa watu mbali usiku na wakala mazao yake. Na Sisi tulikuwa tunaijua hukumu iliyo khusiana na kesi hiyo. Kisa cha hiyo hukumu: Mbuzi waliingia usiku mmoja katika konde ya mtu, wasibakishe kitu. Daud akahukumu kuwa wale mbuzi wawe wa mwenye konde kulipia khasara yake. Suleiman akatoa hukumu nyengine, akasema: Mbuzi wale wabakie mkononi mwa mwenye konde mpaka itapo mea tena mazao yake, na avumilie kwa yaliyo mpata. Na baada yake warejesheane.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kumbuka Nabii wa Allah Mtukufu Dâwûd na mwanae Sulaymân, ewe Mtume, walipotoa uamuzi juu ya kesi iliyoletwa na wagomvi wawili, kondoo wa mmoja wao waliharibu mimea ya mwingine, walienea kwenye mimea hiyo kipindi cha usiku wakaiharibu. Dâwûd alitoa uamuzi kwamba wale kondoo wawe ni milki ya mwenye mimea wakiwa ni badala ya mimea yake iliyoharibiwa, kwa kuwa thamani ya viwili hivyo ni sawa. Na sisi tuliushuhudia uamuzi wao, haukufichamana kwetu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net