Al-Anbiyaa 21:77
الأنبياءوَنَصَرْنَـٰهُ مِنَ ٱلْقَوْمِ ٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَآ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ قَوْمَ سَوْءٍ فَأَغْرَقْنَـٰهُمْ أَجْمَعِينَ
Na tukamnusuru kutokana na watu waliozikanusha Ishara zetu. Hakika hao walikuwa watu wabaya. Basi tukawazamisha wote.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tukamnusuru na watu walio zikanusha Ishara zetu. Hakika hao walikuwa watu wabaya. Basi tukawazamisha wote. [77]
[77] Tukamlinda kwa nusura yetu na vitimbi vya kaumu yake walio zikanusha Ishara zetu zenye kuthibitisha Utume wake. Hakika hao walikuwa watu wa shari. Basi tukawagharikisha wote!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tukamnusuru na vitimbi vya watu waliozikanusha alama zetu zenye kuonesha ukweli wake. Kwa haki, wao walikuwa ni watu wa ubaya, na hivyo basi tuliwazamisha wote kwa mafuriko.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net