Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 76

Al-Anbiyaa 21:76

الأنبياء

وَنُوحًا إِذْ نَادَىٰ مِن قَبْلُ فَٱسْتَجَبْنَا لَهُۥ فَنَجَّيْنَـٰهُ وَأَهْلَهُۥ مِنَ ٱلْكَرْبِ ٱلْعَظِيمِ

Maana

Na Nuhu alipoita zamani, nasi tukamuitikia, na tukamwokoa yeye na watu wake kutokana na shida kubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Nuhu alipo ita zamani, nasi tukamuitikia, na tukamwokoa yeye na watu wake kutokana na shida kubwa. [76]

[76] Na hapa tumjaje Nu'h kabla ya Ibrahim na Luu't, pale alipo muomba Mola wake Mlezi, aisafishe nchi kwa kuondoa waovu tukamuitikia ombi lake, tukamuokowa yeye na wale walioamini katika watu wake, kutokana na shakawa (shida) ya kimbunga kikubwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na mkumbuke Nûḫ, ewe Mtume, alipomuita Mola Wake kabla yako na kabla ya Ibrãhîm na Lûṭ, tukaitika mwito wake na tukamuokoa, yeye na watu wake waliomuamini, na makero makubwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net