Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 79

Al-Anbiyaa 21:79

الأنبياء

فَفَهَّمْنَـٰهَا سُلَيْمَـٰنَ ۚ وَكُلًّا ءَاتَيْنَا حُكْمًا وَعِلْمًا ۚ وَسَخَّرْنَا مَعَ دَاوُۥدَ ٱلْجِبَالَ يُسَبِّحْنَ وَٱلطَّيْرَ ۚ وَكُنَّا فَـٰعِلِينَ

Maana

Basi tukamfahamisha Suleiman. Na kila mmoja wao tulimpa hukumu na elimu. Na tuliifanya milima na ndege kuwa pamoja na Daud imnyenyekee na imtakase Mwenyezi Mungu. Na Sisi ndio tulioyafanya hayo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Tukamfahamisha Suleiman. Na kila mmoja wao tulimpa hukumu na ilimu. Na tuliifanya milima na ndege kuwa pamoja na Daud imnyenyekee na imtakase Mwenyezi Mungu. Na Sisi ndio tulio fanya hayo. [79]

[79] Basi tulimfahamisha Suleiman hiyo fatwa. Na wote wawili tuliwapa hikima na ilimu ya maisha na mambo yake. Na tulimfanyia Daud pamoja na milima it'ii na imtakase Mwenyezi Mungu kama alivyo kuwa anamtakasa yeye Daud na kila lisio kuwa linamwelekea Mwenyezi Mungu. Na kadhaalika tuliwafanya ndege hivyo hivyo wamsabihi Mwenyezi Mungu pamoja naye. Na tulifanya hayo kwa uweza wetu usio shindika.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Tukamfahamisha Sulaymân kuzingatia maslahi ya pande mbili na kufanya uadilifu, akatoa uamuzi kwamba yule mwenye kondoo ashughulike kutengeneza mimea iliyoharibika na kumalizika kwa muda maalumu ambapo katika muda huo yule mwenye mimea ajifaidishe kwa manufaa ya kondoo, kama vile maziwa, sufi na mfano wake, na baadaye kondoo warudi kwa mwenyewe na mimea irudi kwa mwenyewe, kwa kuwa thamani ya mimea iliyoharibiwa inalingana na manufaa ya wale kondoo. Na kila mmoja kati ya Dâwûd na Sulaymân tulimpa busara na ujuzi. Na tulimfanyia Dâwûd wema wa kumdhalilishia majabali yakawa yanaleta tasbihi anapoleta tasbihi, na vilevile ndege wakawa wanaleta tasbihi, na sisi tulikuwa ni wenye kulifanya hilo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net