Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 73

Al-Anbiyaa 21:73

الأنبياء

وَجَعَلْنَـٰهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا وَأَوْحَيْنَآ إِلَيْهِمْ فِعْلَ ٱلْخَيْرَٰتِ وَإِقَامَ ٱلصَّلَوٰةِ وَإِيتَآءَ ٱلزَّكَوٰةِ ۖ وَكَانُوا۟ لَنَا عَـٰبِدِينَ

Maana

Na tukawafanya maimamu wakiongoa watu kwa amri yetu. Na tukawafunulia watende heri, na washike Sala, na watoe Zaka; na walikuwa wanatuabudu Sisi tu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tukawafanya maimamu wakiongoa watu kwa amri yetu. Na tukawafunulia watende kheri, na washike Swala, na watoe Zaka; na walikuwa wanatuabudu Sisi tu. [73]

[73] Na tukawafanya ni Manabii wakiwaendea watu, wakiwaongoa kwenye kheri kwa mujibu wa tulivyo waamrisha. Na tukawaonyesha vitendo vyema, na kudumisha Swala kama inavyo faa, na kutoa Zaka. Na wakawa wanatunyenyekea na kutusafia ibada Sisi tu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na tukamfanya Ibrãhîm, Isḫâq na Ya‛qûb kuwa viongozi wa watu, wanawalingania wamuabudu Yeye na kumtii kwa idhini Yake Aliyetukuka, na tuliwaletea wahyi ukiwaamrisha kufanya mema ya kuzifuata kivitendo sheria za Manabii, kusimamisha Swala kwa njia zake na kutoa Zaka. Na wao walizifuata amri hizo na walikuwa watiifu kwa Allah Mtukufu Peke Yake bila Mwingine.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net